JAMII MATATANI

JAMII MATATANI

Taarifa Mpya Yadhihirisha Jinsi Benki ya Dunia Ilivyoshindwa Kulinda Kanuni Zake Zinazolinda Haki za Binadamu Tanzania
Women threatened by RUNAPA’s expansion in Mbarali District
  • Taarifa mpya yaonyesha kwa kina Benki ya Dunia ilivyoshindwa kurekebisha makosa yake kufuatia ukatili uliopindukia dhidi ya binadamu uliyosababishwa na mradi wake wa utalii Tanzania.
  • Pamoja na Mpango Kazi wa Utawala (MAP) wenye lengo la kushughulikia madhara yaliyotokana na mradi baada ya mradi huo kufungwa, Benki ya Dunia inaendelea kushindwa kutetea jamii zinazokumbana na mauaji, vitisho vya kufukuzwa kutoka ardhi zao, na zuio la riziki.
  • Askari wa TANAPA waliofadhiliwa na Benki ya Dunia wanaendeleza ugaidi dhidi ya wanavijiji huku serikali ya Tanzania ikikiuka ahadi yake ya kuruhusu zaidi ya watu 84,000 ambao vijiji vyao viliathiriwa na upanuzi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kinyume cha sheria kuendelea na maisha yao ya kila siku.
  • Ni lazima Benki ya Dunia iwajibishwe kwa kufadhili mradi potofu sehemu isiyofaa na ni lazima ichukue hatua haraka kupunguza maumivu na kulinda haki ya uzalishaji wa vijiji vilivyodhurika.

OAKLAND, CA –Vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) viko hatarini kutokana na askari katili waliofadhiliwa na Benki ya Dunia. Uwajibikaji Sasa  – Jamii za kiTanzania Zilizoumizwa na Mradi Uliofadhiliwa na Benki ya Dunia, taarifa mpya ya Oakland Institute report, inaweka hadharani dhulma dhudi ya binadamu unaotokana na Benki ya Dunia kushindwa kurekebisha janga iliyosababisha. 

Kama ilivyobaishwa na Taasisi ya Oakland, Mradi wa Kukuza Maliasili na Uralii (REGROW) ulipelekea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kupanuliwa kimabavu, ulisababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, kuvurugwa kwa uzalishaji, na mpango wa kuhamisha halaiki kwa nguvu. Hata Idara ya Upepelezi ya Benki ya Dunia ilibaini uhalifu huu kwenye taarifa yake iliyochapishwa Septemba 2024.  Uwajibikaji Sasa inaeleza kwa kina jinsi Benki ya Dunia inavyochelewa kuchukua hatua stahiki kurekebisha ukiukwaji wa sera zake yenyewe za kulinda banadamu uliyopelekea uhalifu huu unaoendelea.

“Taarifa hii siyo tu inadhihirisha ufadhili huu batili wa Benki ya Dunia, lakini pia inaonyesha namna taasisi hiyo isivyo na uwajibikaji ikizingatiwa kushindwa kwake kurekebisha makosa yake kwa kila hatua. Utawala wa Benki ya Dunia ulikiri kusababisha janga hili – na bado, umewatelekeza wanavijiji wahanga huku ukiukwaji wa haki za binadamu na kuzuiwa kwa uzalishaji ukiendelea bila kikomo,” anasema Anuradha Mittal, Mkurugenzi Metendaji wa Taasisi ya Oakland.

Taarifa inadhihirisha jinsi ufadhili wa Benki ya Dunia ulivyowezesha serikali kuongeza ukubwa wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa zaidi ya hekta milioni moja kupitia Gazeti la Serikali Namba 754 la Octoba 2023 bila ridhaa ya wanaoishi kwenye ardhi hiyo. Hii inawaweka katika wakati mgumu zaidi ya watu 84,000 kutoka kwenye vijiji 28 na kusababisha hasara ya zaidi ya dola za Kimarekani 70 milion kwa wakulima na wafugaji – maumizu yakiongezwa na mauaji na ukatili kwenye mikono ya askari waliofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Kati ya 2017-2024, Benki ya Dunia iliwapa nyenzo na kuwaimarisha askari wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), ikapelekea shirika hilo kufanya ukatili dhidi ya wenyeji. Wanajamii wameuwawa kikatili, wengine wamepotezwa, kuteswa, na ugumu wa kiuchumi – haya yote yakisababishwwa na Benki ya Dunia kutokuwa na uangalizi wa karibu na  makini wa miradi inayofadhili. 

Mradi wa REGROW ulifadhiliwa na Benki na Benki ya Dunia ulifungwa rasmi mnamo Novemba 6, 2024. Mnamo April 1, 2025, Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia iliidhinisha Mpango Kazi (MAP) wenye lengo la kutatua makosa ya mradi huo yaliyobainishwa na taarifa ya uchunguzi iliyoandikwa na Idara ya Upelelezi ya Benki ya Dunia. Badala ya kutatua madhara yalibainishwa na Idara ya Upelelezi na kushughulikia matakwa ya jamii wahanga, MAP imechagua kile kinachoita riziki mbadala na kuafiki ahadi yenye mashaka ya serikali kuwa wanavijiji waliingiliwa na hifadhi hawatahamishwa bali wataendelea na ufugaji, uvuvi na kilimo.

Karibu mwezi mmoja baada ya ahadi hiyo, mnamo April 26, 2025, mvuvi Hamprey Mhaki, mwenye umri wa miaka 27 alipotezwa baada ya kupigwa risasi na askari wa hifadhi ndani ya Bonde la Ihefu. Mnamo Mei 7, askari wa hifadhi waliwamiminia risasi wafugaji katika Kijiji cha Iyala, na kumuua Kulwa Igembe mwenye umri wa miaka 20, na kukamata ng’ombe zaidi ya 1,000 ambayo ni pigo jingine kwa wafugaji. 

Benki ya Dunia ilisema kuwa unajitolea kufanya kazi na serikali ya Tanzania “kusaidia jamii inayoishi ndani na jirani na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha katika jitihada ya uhifadhi na maendeleo, ikiwa ni pamoja na kupunguza migogoro na ukatili hifadhini na kutoa fursa mbadala ya riziki.” Mauaji ya hivi karibuni, ukamataji wa mifugo, na kukataza kilimo, vinaumbua udhaifu wa ahadi ya Benki ya Dunia. Vijiji vingi vimeamrishwa vihame – na moja kwa moja kucontradicting hakikisho la awali la serikali kutovihamisha. Pamoja na kudai kwamba inasimamia utelelezaji wa MAP, utawala wa Benki ya Dunia imeachia serikali ile ile iliyosababisha ukatili huu kuchunga ukatili wenyewe. 

“Endapo ahadi ya msingi ya kuwaruhusu wanavijiji kuendelea na maisha ya ki la siku haitaheshimiwa, maisha ya wanavijiji yatakuwa hatarini. Jamii wahanga walitegemeea Benki ya Dunia kusimamia MAP. Wameshtushwa mno na jibu la Benki ya Dunia kwamba aliewaumiza atawatendea haki. Kutokana na taarifa za ukiukwaaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Tanzania, hii ni sawa na kuruhusu fisi aingie katika zizi la mbuzi,” alihitimisha Mittal. 

Muda wa kurekebisha madhara ya mradi huu umepita mno. Mwanakijiji mmoja mhanga anasema, “Tunalilia ardhi yetu…tunataka kuwa huru. Hatutaki kuhama na Benki ya Dunia izuie serikali isichukue ardhi yetu. Mateso yetu yanatokana moja kwa moja na Benki ya Dunia. Tunataka kuwa huru.” 

Country
Additional Languages
Image
Lives on hold: young women in Mbarali District